HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

Kuweka Amana

Utangulizi

Amana ni fedha anayoiweka mwanachama kwa lengo la kujiwekea akiba inayoweza kumsaidia badae. Amana ni fedha inaweza kuwekwa muda wowote na kutolewa ama kupunguzwa muda wowote.

  1. Aina Za Amana

Ili kuendesha Chama kibiashara, Hai Teachers Saccos imeweka makundi mawili (2) makuu ya aina za amana ambayo ni;-

  (a) Amana ya Kawaida

  (b)  Amana ya Muda Maalum 

(a) Amana ya Kawaida

Amana ya kawaida ni fedha anayoiweka mwanachama muda wowote na anaweza kuitoa muda wowote anapohitaji.

  (b)  Amana ya Muda Maalum

Kwa upande mwingine amana ya muda maalum ni amana ambayo Mwanachama aningia makubaliano au mkataba na Chama kutoichukua amana yake kwa muda uliokubaliwa kwa ahadi ya Chama kumlipa riba ndani ya kipindi cha makubaliano.

Viwango vya riba katika amana ya muda maalum vitatokana na hali ya biashara pamoja na viwango vya soko la fedha ambapo kwa Hai Teachers Saccos (1993) Limited hutolewa kuanzia asilimia tano (5)%

  1. Taratibu za Uwekaji Amana

Chama kina fomu maalum kwa ajili ya Mwanachama kujaza na kuweka amana. Kuna fomu tofauti za Amana ya kawaida na amana ya muda maalum.

Kuweka Amana

  • Amana za kawaida – KUANZIA 10,000 hadi 100M
  • Amana za mda maalumu kuanzia M 5 HADI 100M
Scroll to Top