HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

Kununua Hisa

KUHUSU HISA

  1. Maana Ya Hisa

Sheria ya Ushirika na. 6 ya mwaka 2013 kupitia kifungu cha 41 inatambua uwepo wa Mwanachama (member) na Mteja (client), ikiwa mwanachama ni yule aliyenunua hisa ndani ya chama wakati mteja ni yule anayetumia huduma za akiba na amana ndani ya Chama.

HISA NI UWEKEZAJI WA MSINGI KABISA KWA MWANACHAMA. Hisa humfanya mwanachama kuwa mmilikia halali wa SACCOS.

2. AINA ZA HISA
Kuna aina mbili za hisa ambazo mwanachama anaweza kuchangia ambazo

  (a) Hisa Za Lazima
Hisa za lazima ndiyo hisa za umiliki wa Chama, ni kiwango cha chini cha hisa ambazo kila mwanachama anatakiwa kumiliki ndani ya Chama. Hadi sasa hisa za msingi kwa HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) LIMITED ni kama ifuatavyo;

   (a)  Kiwango Cha Awali Cha Idadi Ya Hisa ni 5 zenye thamani ya Sh  50,000/= (Pindi mwanachama anapojiunga na chama)
   (b)  Thamani Ya Kila Hisa Ni Tsh 10, 000/=
   (c) Hisa za msingi kwa Kila Mwanachama Ni Tsh 500, 000/= ambazo kila mwanachama atahitajika kuzikamilisha ndani ya miaka miwili tangu awe mwanachama .

     (b) Hisa za ziada

ni zile ambazo mwanachama atachangia juu ya hisa za msingi. Aidha mwanachama anaweza kuchangia hisa za ziada mpaka 20% ya Hisa zote za Chama (HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) LIMITED).

Scroll to Top