Huduma za Akiba
Utangulizi
Akiba ni fedha anazochangia mwanachama ili kuwa na sifa ya kupata huduma za mikopo. Kulingana na masharti ya chama fedha hii ni mali ya mwanachama ila hairuhusiwi kutoka hadi pale mwanachama anapokoma uwanachama. Aidha mwanachama wa Hai Teachers Saccos atapaswa kuandika notisi na akiba zake atarejeshewa baada ya siku 90 tokea kupokelewa na notisi hiyo.
Aina Za Akiba
Hai Teachers Saccos Limited ina makundi makuu mawili ya Akiba
(a) Akiba Za Lazima
Akiba ya lazima inamfanya mwanachama kuwa na sifa ya kupata huduma ya mikopo hadi mara tatu ya akiba. Ambapo kiwango cha chini cha kuchangia akiba ni Tsh 30,000 kila mwezi. Kiwango hiki kinaweza kinaweza kubadilika kama inavyoelekezwa kwenye Masharti ya Chama
(b) Akiba Za Hiari
Akiba ya hiari ni akiba anayojiwekea mwanachama kwa malengo mahsusi na akiba hii inaweza kutolewa ama kupunguzwa muda wowote kama hakijatumika kama dhamana kwenye mkopo.
Aina ya Mazao ya Akiba ya Hiari
Mwanachama anaweza kuweka akiba yake ya hiari katika moja ya mazao yafuatayo:-
Akiba Ya Malengo Maalum
(a) Akiba Ya Watoto
(b) Akiba Ya Elimu
(c) Akiba Ya Sikukuu
(d) Akiba Ya Wastaafu
(e) Akiba Ya Jamii
(f) Akiba Ya Mshahara
FAIDA ZA KUWEKA AKIBA
- Faida Juu Ya Akiba:
Kila mwaka HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) LIMITED kupitia Mkutano Mkuu huweka kiwango cha faida juu ya akiba za wanachama ili kuwezesha ongezeko la thamani ya akiba za mwanachama. Kwakuwa hii ni gharama ya kifedha kwenye Chama itakuwa inabadilika kila mwaka kutokana na mwelekeo wa makisio ya mapato na matumizi. Endapo Mwanachama akikoma kuwa mwanachama wa HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) LIMITED atatakiwa kuandika notisi na akiba zake atarejeshewa baada ya siku 90 tokea kupokelewa na notisi hiyo.
- Kumwezesha mwanachama kupata mkopo
- Akiba humwezesha mwanachama kujiiimarisha kifedha katika maisha yake ya uzeeni.
- Akiba hutumika kama dhamana wakati wa kukopa