HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

HAI TEACHERS' SACCOS (1993) LIMITED

Huduma za mikopo

Hai Techers Saccos (1993) Limited  inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya maendeleo , Mikopo ya dharura na Mikopo ya salary advance.

1. Mikopo ya maendeleo

Hii ni mikopo amabayo chama huwapatia wanachama wake kwa madhumuni ya kuwawezesha wanachama wake kupata maendeleo ya kiuchumu katika familia yake kama vile kufanikisha ujenzi wa nyumba, kilimo, kununua kiwanja n.k

 Mikopo hii hutolewa kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:

  • Mwanachama ana uhuru wa kukopa kiwango ambacho hakizidi mara nne (4) ya akiba kulingana na mahitaji ya mwanachama.
  • Mwanachama ataruhusiwa kukopa tena iwapo atakuwa amemaliza mkopo wa awali, au amerejesha moja ya tatu (1/3) la deni la awali.
  • Kiwango cha juu cha mkopo kitategemea uwezo wa mshahara wa mwanachama husika.
  • Riba kwa mkopo wa maendeleo ni asilimia 0.91 kwa mwezi kwa baki ya mkopo.
  • Muda wa juu wa marejesho ya mkopo ni miezi sitini (60)
  • Kiwango cha juu cha kukopa ni Mil 25,000,000

2. Mikopo ya dharura – hadi million 2M

 Hii ni aina ya mikopo inayotolewa pale mwanachama anapopata dharura amabayo ni ya lazima na hajamaliza mkopo mwingine aliopewa. Aidha mwanachama atapewa mkopo huu hata kama anadaiwa mkopo mwingine.

Katika mkopo huu mwanachama ataweza kukopeshwa hadi Tsh 2M kulingana na uwezo wa kurejesha wa mwanachama husika lakini pia tabia ya kulipa ya mwanachama husika.

3. Mikopo ya Salary Advance

 Mikopo hii hutolewa kwa madhumuni ya kumwezesha mwanachama kujikimu pale ambapo mshahara wake haujatoka au amepata changamoto ambayo imepelekea mshahara wake kushindwa kutatua changamoto hiyo. Mkopo huu mwanachama anaweza kuupata hata kama ana mkopo wa maendeleo.

Mkopo huu unarejeshwa kwa mwezi mmoja tuu kwa riba ya asilimia 3% TUU

Scroll to Top