Karibu
HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) Limited, Tunajivunia kuwa ushirika wa kifedha ambao unawawezesha wafanyakazi wa umma na kutoka mashirika binafsi kutimiza malengo yako ya kiuchumi.Tumejitolea kutoa huduma bora, kwa wakati, riba nafuu, na fursa za uwekezaji kwa wanachama wetu. Jiunge nasi leo, na tufanye kazi kwa pamoja kutimiza ndoto zako.HAI TEACHERS’ SACCOS (1993) LIMITED ni moja ya saccos kubwa iliyoanzishwa na walimu chini ya sheria ya ushirika Na 15 ya mwaka 1991 na kusajiliwa kwa namba KLR 440. Hai Teachers’ saccos (1993) Limited ilianzishwa mwaka 1993 ikiwa na wanachama 20 na mtaji wa Tsh 100,000 ikiwa na lengo la kuunganisha watumishi wa umma kutengeneza ushirikika wa kifedha utakaowezesha watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa kutatua changamoto zao za kifedha. Hadi kufikia Dec, 2024 hai teachers saccos ina Jumla ya wanachama 942.